ItsBellazWorld

Fashion,Health and Beauty

Jumapili, 20 Desemba 2015

Urembo: Jinsi ya kuzuia na kuondoa wrinkles

Hello world,so leo nimeona niwape tips jinsi ya kufanya kuwa na ngozi nzuri inayovutia.Najua wengi wetu labda tunajua ninachotaka kukisema ila pia si ajabu kuwa kuna ambao bado hawajui hivyo wanaweza kuwa wakanufaika na hii topic.Nitaanza mara moja ili nisiwachoshe kwa maneno mengi.

MAHITAJI
Yai,asali,sukari laini ya unga,limao,manjano,nyanya iliyoiva vizuri lakini ngumu,bakuli mbili,liwa,sabuni,taulo laini na safi na moisturizer.

JINSI YA KUFANYA
Safisha vizuri uso kisha kausha kwa taulo,usiache maji yakaukie yenyewe usoni,sio vizuri.Chukua nyanya uliyoisafisha vizuri kisha ikate katikati kisha inyunyuzie sukari,halafu sugua nayo usoni taratibu sana bila kujichubua ,sugua kama unachora maduara kuanzia kidevuni kwenda kwenye paji la uso,usianzie juu kwenda chini siku zote anzia chini kwenda juu.Kitendo hiki /exfoliation husaidia kuondoa ngozi zilizokufa,kufungua vitobo katika ngozi,hivyo ngozi kupumua vizuri maana ngozi isipoingiza hewa mtu anaweza kupata chunusi.Ukishafanya hivyo kwa kama dk 2 then acha ibakie hivi hivi usoni then;

Chukua yai lipasue katikati ukihakikisha kuwa kiini hakivurugiki,kishatenganisha ute mweupe kwenye bakuli lake na kiini kwenye bakuli lake,Kisha chukua bakuli lenye kiini weka manjano,asali,matone ya limao na liwa kisha koroga upate mchanganyiko unaoona utanata usoni bila kuchuruzika.Kila kitu pima kulingana na jinsi wewe unavyoona itatosha kukupatia mchanganyiko usio mwingi wala kidogo sana na wala usio mgumu wala mwembamba sana.

Then,safisha uso kuondoa zile nyanya na sukari,jikaushe then jipake huu mchanganyiko ukae nao kwa dk 10-15 au zaidi kama muda unaruhusu.

Baada ya hapo,safisha vizuri uso wako huku ukisugua sugua kama kuna ngozi zilizokufa zilizobakia zitoke zote kisha jikaushe halafu;

Chukua lile bakuli lenye ute mweupe wa yai,(hakikisha kiini hakijaingia humu hata kidogo),chukua uma kisha pigapiga huo ute hadi uwe kama povu halafu jipake usoni kwa wingi mara moja kisha toka nje upigwe na upepo ambao utasaidia kukausha kwa haraka huo ute.Kadiri ute utakavyokua ukikauka usoni mwako utaona kuwa ngozi ya uso wako inajivuta na kuwa tight.Kaa na huu ute kwa dk 10-15 kama unaweza kukaa nao zaidi ni vizuri.Hii inasaidia kukaza misuli ya uso hivyo kuzuia wrinkles au kama zipo inasaidia kuziondoa maana wrinkles huja pindi misuli ya uso inapokua imelegea.

Baada ya hapo safisha uso paka moisturizer/lotion yako.

Ukifanya hivi kila wiki mara moja baada ya mwezi utaona jinsi ngozi yako inavyobadilika,ila hata siku ya kwanza utaona ngozi yako haiko kama ilivyokua kabla ya kufanya hivi.

NOTE
Vipo vitu vingi sana vya asili vinavyotumika na sio mbaya kuongeza vitu vingine kama kitunguu saumu,matango,wengine maziwa,unga wa dengu na vingine vingi ila kuna watu wanachanganya pia na mafuta ya mawese,kabla ya kuchanganya mawese kwenye mchanganyiko wako ni lazima uwe na uhakika wa asili mia moja kuwa ngozi yako haitareact vibaya baada ya kujipaka haya mafuta.Kuna ngozi hazitaki mafuta,hivyo mtu unaweza kujipaka mawese ukashangaa umepata chunusi za kufa mtu.

Okay,hope kuna waliofaidika.

Imechapishwa na Unknown kwa 23:40 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Jumamosi, 19 Desemba 2015

Ngozi zenye mafuta na jinsi ya kuzitunza



Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kuridhi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta
Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.
2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.
7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.
9. Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.
Imechapishwa na Unknown kwa 23:10 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Jumatano, 16 Desemba 2015

Beauty & Tips

Girls dream!!  Be a fashionable kiosk of your own style, we both love fashion mostly attention, what does what, who went wear, doesn't matter as long as you look GOOD!!!! 
And guys do you want to kill it?? why not try a different style look smart that's every girl's dream. 
Go with trend!!1 























Imechapishwa na Unknown kwa 13:25 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Beauty & Tips!!!



WHY NEED A MAKE UP ARTIST????
be your own artist!!!! learn how to do your own make up at home and look Amaiiiiiizing!!!!
 learn step by step how to do your own make. 






Imechapishwa na Unknown kwa 12:49 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Jumapili, 13 Desemba 2015

What your kid should wear to go with style












Imechapishwa na Unknown kwa 11:30 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Art of kitenge!!! that trends







Imechapishwa na Unknown kwa 10:57 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Decorate your house in a stunning epic!!!











Imechapishwa na Unknown kwa 10:54 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Afro!! A Stlye that will never go out of fashion..





Imechapishwa na Unknown kwa 10:50 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest
Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Nyumbani
Jisajili kwenye: Machapisho (Atom)

Kunihusu

Unknown
Tazama wasifu wangu kamili

Kumbukumbu la Blogu

  • ►  2016 (13)
    • ►  Septemba (1)
    • ►  Juni (1)
    • ►  Aprili (2)
    • ►  Februari (5)
    • ►  Januari (4)
  • ▼  2015 (12)
    • ▼  Desemba (8)
      • Urembo: Jinsi ya kuzuia na kuondoa wrinkles
      • Ngozi zenye mafuta na jinsi ya kuzitunza
      • Beauty & Tips
      • Beauty & Tips!!!
      • What your kid should wear to go with style
      • Art of kitenge!!! that trends
      • Decorate your house in a stunning epic!!!
      • Afro!! A Stlye that will never go out of fashion..
    • ►  Novemba (4)
Mandhari ya Safiri. Inaendeshwa na Blogger.